Rain is not only drops of water. It is the LOVE of sky 4 earth. They never meet each other but send LOVE this way. Enjoy the LOVE of nature.
Friday, August 24, 2012
Diamond aitwa Ikulu
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete amemuita ikulu mwanamuziki anayefanya vizuri kwa sasa kwenye Bongo Fleva, Nasibu Abdul Jumaa ‘Diamond Platnumz’ na kumpa jukumu maalum, Ijumaa linairusha hewani.
Kwa mujibu wa Diamond, juzikati ‘prezidenti’ alimwita ikulu Magogoni, Dar es Salaam na kumpa shavu la kwenda kufanya shoo kwenye mkutano maalum utakaofanyika Washington DC nchini Marekani hivi karibuni.
“Yaa, rais aliniita akaniambia kuna shoo natakiwa kwenda kufanya Marekani. “Kwa mara ya kwanza nitasafiri nje ya nchi na madensa wangu wanne na msemaji mmoja. Sasa hivi hawataki kutembea na kupanda magari wasije wakakosa hiyo safari,” alisema Diamond na kuongeza kuwa baada ya kuumwa, mawazo aliyaweka kwenye mchongo huo hivyo mambo mengine yataendelea ikiwa ni pamoja na kufanya kolabo na mwanamuziki wa kimataifa wa Nigeria, J. Martins.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment