Rain is not only drops of water. It is the LOVE of sky 4 earth. They never meet each other but send LOVE this way. Enjoy the LOVE of nature.
Sunday, August 19, 2012
Simba wanyakua ubingwa wa Super8 mbele ya Mtibwa sugar.
Kikosi cha Simba B jana jioni kilipata ubingwa wa ligi ya super8 baada ya kuifunga timu ya mtibwa sugar kwa jumla ya magoli 4 kwa 3. Kikosi hicho cha simba B kikiwa chini ya kocha Suleiman Matola kilifanikiwa kuingia fainali hiyo baada ya kuifunga Azam fc kwa magoli 2 kwa 1. Nao mtibwa sugar waliifunga timu ya mafunzo toka zanzibar kwa jumla ya magoli 5 kwa 1. Katika mchezo huo wa fainali, simba walionekana kutakata na kuonyesha kandanda safi mbele ya mashabiki wao. Kikosi hicho cha simba kilifanikiwa pia kutoa mchezaji bora kwa ufungaji na golikipa bora ambao walipata tzs mil 2.5 kila mmoja. Bingwa wa mashindano hayo amejinyakulia kitita cha tzs mil 40 huku mshindi wa pili akiambulia mil 20.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment